Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Juma Homera akizungumza na wananchi wa kata ya Katumbasongwe wakati wa kukabidhi misaada kwa wahanga wa mafuriko Kyela.
Wananchi wa kata ya katumbasongwe wakiwa wanamsikiliza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi wa kata ya Katumbasongwe kwa niaba ya wananchi wote wa wilaya ya kyela, walioathirika na mafuriko, yalitokea wilayani hapa usiku wa kuamkia tarehe 27.4.2022 hadi 28.4.2022 huku katumba songwe ikiwa ni miongoni mwa kata 17 zilikumbwa na mafuriko hayo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa misaada hiyo Mheshimiwa Homera ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya waziri Mkuu TAMISEMI,Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kyela pamoja na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kyela kwa juhudi kubwa wanazozifanya za kuwasidia wananchi wa Kyela.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amewaeleza wananchi hao kuwa, misaada iliyotolewa ni magodoro, mablanketi sukari na mafuta ya kupikia, na amesema misaada hiyo sio ya Katumbasongwe pekee, bali ya wananchi wote walioathiriwa na mafuriko, lakini pia amesema, ili kunusuru mafuriko ya mara kwa mara, seriklai kwa kushirikiana na nchi jirani ya Malawi ina mpango wa kujenga bwawa kubwa ili kuweza kuwanusuru wananchi na mafuriko.
Aidha ametoa onyo kwa kamati ya maafa kuhakikisha kuwa hakuna upotevu wowote unaojitokeza kwenye misaada inayotelewa, Na kuwaomba viongozi wa kata, vijiji, vitongoji wagawe vitu hivyo kwa haki na sio kwa upendeleo ndani ya siku 2. Vilevile amewahidi wananchi wa kyela kuwa ujenzi wa madaraja utaanza hivi karibuni ili kurejesha mawailiano ya kata na kata.
Nae Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Kyela ASCP Ismail Mlawa amemueleza Mheshimiwa mkuu wa mkoa kuwa atasimamia vyema ugawaji wa misaada iliyotolewa, na kuwahidi wananchi kuwa, watu wote walioathirika na mafuriko na kuandikishwa watapatiwa msaada huo, Aidha amesema wakazi 46 wa kitongoji cha lugome kata ya Mwaya kwa hiari yao wameiandikia Ofisi ya Mheshiwa mkuu wa wilaya kuomba kuhamishiwa katika mazingira salama.
Pamoja na hayo Mkuregenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ambae ndie mwenyekiti wa kamati ya maafa wilaya Ndugu Ezekiel Magehema amesema jumla ya kaya 284 zimeathiriwa zaidi na mafuriko kwani nyumba zao zilibomoka kabisa na jumla ya watu 1,193 ikiwa wanaume ni 447 na wananwake 746 wameathiriwa sana.
Aidha amesema nyumba 249 zimepata athari ndogo ndogo kama kupata nyufa huku mashamba ya mpunga jumla ya hekta 10,616 zilizama na maji, pia mifugo yaani ng’ombe 101, nguruwe 200 na kuku 2,061 wote walisombwa na maji.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela (katikati) akiwa anamsikiliza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati wa ugawaji wa misaada kwa wahanga wa mafuriko Kyela.
Mathalani athari kubwa ya miundombinu kama barabara madaraja na baadhi ya shule zilingiliwa na maji na kulazimika kufungwa kwa muda mpaka maji yalipopungua na kupelekea jumla ya shule 27 za msingi na shule 5 za sekondari kufungwa kwa muda.
Madaraja ya waenda kwa miguu katika mto kiwira yameharibiwa kabisa na mafuriko, mfano daraja la Ibungu na daraja la Mwalisi ambayo yatahitaji matengenezo.
Magehema amesema kuwa kamati ya maaafa imebaini kuwa mahitaji ya kiutu yanayohitajika Zaidi ni kama chakula, magodoro, mashuka, blaketi, neti za mbu na dawa za kutibu maji ya kunywa.
Nae Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Kyela ndugu Ally Jumbe Kinanasi amewaambia wananchi kuwa, serikali ya awamu ya sita inaendelea kufanya juhudi mbalimbali ili kuboresha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko na kuwataka wawe na imani na serikali yao.
Mwisho baadhi ya wananchi walitoa shukurani zao kwa niaba ya wananchi wengine kwa KUishukuru Serikali ya awamu ya sita, kwa kuwajali na kuwasaidia wananchi hao katika kipindi wanachopitia baada ya mafuriko kutokea.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0756944794
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa