Haya yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule kingamkono, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Itunge hapa wilayani Kyela tarehe 30/08/2021.
Akizungumza na wananchi hao, Mheshimiwa Kingamkono amewahakikishia wananchi hao kwamba kiasi cha shilingi 250,000,000/= tayari zimeshawekwa katika akaunti benki kwa ajiri ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Itunge, Hii ikiwa na lengo la kutimiza ndoto ya wanaItunge kuwa na kituo cha Afya.
Kwa upande wao wananchi walimhakikishia Mwenyekiti kuzisimamia pesa hizo, pia walikubaliana kuanza kutoa michango ili kusaidiana na serikali katika juhudi za kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kyela na Tanzania kwa ujumla.
Aidha Mheshimiwa Mwenyekiti aliweza kuhudhulia na kufungua mafunzo kwa wanafunzi waliomaliza vyuo, na ambao hawajafanikiwa kupata ajira. Mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Mji mdogo Kyela. Mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya jamii chini ya Mkuu wa idara hiyo ndugu Victor Kabuje. Mafunzo hayo yamelenga kutoa elimu ya kutumia fursa zilizopo hapa wilayani na nje ya wilaya zitakazowasaidia kujiajiri.
Pia Mheshimiwa Mwenyekiti aliahidi kutoa mikopo kwa wanafunzi watakaounda vikundi kwa ajiri ya ujasiriamali. Ikiwa ni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, yanayotengwa kwa ajiri ya kuwakopesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu .
Mwisho Mheshimiwa Katule Kingamkono aliweza kutembelea ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Njisi iliyopo kata ya Njisi, ambapo aliungana na wananchi wapenda maendeleo katika harambee ya ujenzi wa shule hiyo, Na kuwaahidi kuchangia shilingi 10,000,000/= kwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika kata ya Njisi wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa