Wananchi wa Kata ya Ibanda wilayani Kyela Waliojitokeza katika mkutano wa Hadhara na kujionea tripu za mawe zikishushwa kwaajiri ya ujenzi wa shule mpya ya Ibanda Sekondari.
Mbunge wa jimbo la Kyela Mheshimiwa Ally J. Kinanasi ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 2,000,000/= ili kusaidia ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayotarajiwa kuanza kujengwa katika kata ya Ibanda hapa wilayani Kyela.
Akizungumza haya kwa njia ya simu katika mkutano wa hadhara wa kata hiyo, ulioitishwa na Mheshimiwa Katule G. Kingamkono Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Mheshimiwa Mbunge amesema; anafuraha kubwa kuungana na wananchi wa kata ya Ibanda katika suala la maendeleo ya kata hiyo. Na hivyo ameguswa kuchangia kiasi cha shilingi 2,000,000/= ili pesa hiyo ikanunue mifuko 100 ya saruji, na itakayobaki isaidie katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa shule hiyo mpya ya sekondari Ibanda.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, ameitisha mkutano huo wa wananchi katika kata ya Ibanda kwa lengo la kuwatia moyo juu ya ujenzi wa shule hiyo mpya, na katika kuthibitisha hilo aliwataka wananchi hao kushuhudia tripu za mawe zilizokuwa zikiletwa kwa michango yao tayari kwa maandalizi ya ujenzi wa shule hiyo mpya.
Tripu za mawe zikishushwa kwa maandalizi ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Ibanda.
Akiongea kwa furaha kubwa bi.Grace Samweli Mwalunene(mkazi wa ibanda) amesema, kwa sasa anaiona Ibanda mpya, kwani amekuwa akitamani maendeleo yanayofanywa na kata nyingine nyingi za hapa wilayani, ila kwa sasa ni zamu ya Ibanda.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa