Waziri wa nishati Mhe. Dr. Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Kyela tarehe 21/04/2018, katika ziara yake ameahidi kumaliza tatizo la kutokuwa na Kata zisizokuwa na umeme hapa wilayani.
Amesema katika mradi wa REA awamu ya tatu serikali imejipanga kupeleka huduma za Umeme katika Kata mbili ambazo hazikufikiwa na mradi wa REA awamu ya kwanza na ya pili yaani Kata ya Nkokwa na Kata ya lpande.
Akiongea na watumishi wa Serikali na waandishi wa habari,alisema katika Wilaya ya Kyela kuna Kata 33 na baina ya hizo ni Kata mbili tu ambazo hazikupata Umeme.
Hivyo basi kupitia mpango wa Rea awamu ya tatu Kata hizo na vijiji vyake kumi na tatu vitapatiwa Umeme.
Aidha Mhe. Waziri aliwaambia watumishi na waandishi wahabari kuwa Serikali itapeleka Umeme katika taasisi zote za serikali na zisizo za Kiserikali,zikiwemo shule, zahanati, mitambo mbalimbali, makanisa na misikitini.
Lakini pia serikali itapeleka Umeme hadi katika visiwa hata kwa njia mbadala ikiwemo kupitisha Umeme chini ya maji au kwa njia ya sola.
Aidha Mhe. Waziri alipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Ipande, akiwa mwenye furaha kubwa aliwaambia Wananchi kuwa Umeme utaanza kupelekwa katika Kata hizo kuanzia mwezi huu.
Kwani nguzo 200 zilizokuwa zikihitajika zimepatikana ikiwa na transifoma mbili.
Hata hivyo Mhe, Waziri hakusita kuzungumzia matatizo wanayoyapata Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, mfano kukatika kwa Umeme Mara kwa Mara, watu kuchelewa kuunganishwa na huduma ya umeme hata kama wamelipia.
lakini aliwahakikishia Wananchi kuyamaliza matatizo hayo kuanzia sasa.
Mwisho alitoa maagizo kwa Wakurugenzi wote nchini, kuingiza Umeme katika taasisi za kiselikari pindi Umeme unapofika katika taasisi za serikali.
Ziara ya Mhe. Waziri imeleta nuru na kuwapa matumaini kwa Wananchi wa Kyela kuzima taa za Kandili na mishumaa.
Tunaamini hadi kufikia mwaka 2021 Tanzania yetu itakuwa na nuru ya Umeme. Kila raheli Serikali yetu ya awamu ya tano kwa Maendeleo ya kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa kati.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa