Halmashauri ya kyela imeweza kutoa mkopo wa Tsh 1,457,343,755 kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia 2015/2016 hadi 2022/2023 na kati ya mkopo huo kiasi cha Tsh.1,046,548,000 zimeweza kurudishwa na kiasi cha Tsh 410,795,75. Bado hakijarejeshwa kutokana sababu mbalimbali ikiwemo vikundi kusambaratika na wakopaji wengine kukimbia ndani ya wilaya na wengine wanaendelea kufuatilia ili waweze kurejesha fedha hizo ili wakopeshwe wengine.
Hata hivyo utakumbuka mikopo ilisimamishwa na Mhe,Waziri Mkuu na imerejeshwa tena mwaka 2024 ili kuandaa utaratibu mpya wa utoaji mikopo ambao ulikamilika na dirisha kufunguliwa Oktoba 2024
ili kutoa mikopo ambayo itarejeshwa Idara kwa kushirikiana na wawezeshaji kutoka Idara ya fedha na kitengo cha Tehama walitoa maelekezo na uundaji wa kamati mbalimbali kwa kufuata mwongozo mpya ambazo ni;-
Kamati hizi zilipewa mafunzo ya namna ya kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha wanayasimamia na kamati zote na wataalamu wa idara ya Maendeleo ya jamii waliapishwa na Mhe. Hakimu kama mwongozo unavyoelekeza.
UTOAJI MKOPO KWA ROBO YA PILI OKTOBA-DISEMBA,2025
Mkurugenzi Mtendaji alitangaza uwepo a fedha Tsh 991,664,777.00 kwa ajili ya mikopo kwa makundi tajwa hapo juu, ambapo Idara ilianza uhamasishaji kupitia redio za kijamii mikutano ya hadhara na wadau mbalimbali ambapo mpaka Disemba 2024 Halmashauri imepokea maombi ya Tsh. 3,178,066,100.00 yenye vikundi 165 ambapo vikundi vya wanawake 87 navikundi vya vijana 72 ukiacha vikundi vilivyoomba Januari na Februari, Mchakato wa kutoa mkopo umefanyika kwa kuanza kutoa mafunzo ya siku 4 kwa vikundi vyote vilivyoomba. Tulipokea mapendekezo kutoka kata na kamati husika zikapitia na kuhakiki uwepo wa vikundi, hivyo halmashauri yetu mpaka sasa hawa ndio wakopaji na hakuna kikundi hewa.Tunaleta mkopo wa Tsh 816,831,820 ili zikopeshwe vikundi vya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Vijana wanakopeshwa Tsh. 396,665,910 na vikundi vya wanawake Tshs.396,665,910 na Watu wenye ulemavu Tshs.23,500,000. Kwa vikundi ambapo walitengewa 198,332,955.40 kiasi cha Tsh.172,332,955.Ambazo wakopaji hawajapatikana wenye ulemavu zitakopeshwa robo ijayo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
CHANGAMOTO
SHUKRANI
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa