Kurugenzi ya uenezaji wa huduma kutoka TFDA kanda ya mbeya ikiongozwa na ndugu Themistocles Rutta Kahamba, wametembelea wilaya ya Kyela na kutoa elimu mashuleni, juu ya matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu.
Wakitoa elimu hiyo kwa wanafunzi wamesema;
Vipodozi vingi vinavyotumiwa na wananchi hapa nchini, vinasumu kali ambazo zinauwezo mkubwa wa kuathili afya kwa binadamu. Ambapo aliwataka wanafunzi wote kupeleka taarifa wazazi na ndugu wa karibu yao.
Aidha baadhi ya madhara yaliyotajwa ni pamoja na kuwashwa kwa ngozi, macho kutoona vizuri, kupata mtoto mlemavu au aliekufa kabisa, ngozi kutoshoneka ikipata majeraha na saratani.
Aidha baada ya elimu hiyo, ushauri ulitolewa kwa wanafunzi kupeleka ujumbe kwa watumiaji wa vipodozi hivyo. Wakiwataka watumiaji wote wa vipodozi kununua vipodozi vilivyofanyiwa uchunguzi katika maduka yenye vibari vya TFDA.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa