Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi wa Kata ya Makwale Kijiji cha Mpegere Tarehe 9.7.2025.
Miongoni mwa kero zilizoongelewa na Wananchi wa kijiji cha Mpegere ni pamoja na Gharama za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya,ushuru wa kusafirisha mazao na kukosekana kwa Shule ya Msingi.
Akitatua kero ya gharama za Matibabu Mhe.Mkuu wa Wilaya ameuagiza uongozi wa Kijiji kuorodhesha majina ya familia ambazo ziko tayari kusajiliwa kwenye Bima ya iCHF ili Mratibu wa Bima ya Afya (iCHF) kutoka Hospital ya Wilaya ya Kyela awafuate Wananchi kijijini kwa ajili ya kufanya usajili wa Bima.
Bima hiyo ya iCHF inatolewa kwa Tsh. Elfu 30 kwa familia yenye watu 6 yaani Baba, Mama na Watoto wanne,
pia na makundi mbalimbali mfano Bodaboda wao wanakuwa watu 5 Mmoja anakuwa mkuu wa Kaya.Ambapo Bima hiyo ya Familia inatumika Kwa Mwaka Mmoja.
Kuhusu kero ya ushuru wa usafirishaji wa mazao kwa wakulima kutoka nyumbani na kupeleka kwenye Maghala Mhe.Josephine Manase ameuagiza uongozi wa Vijiji na Kata kutoka vibali vya utambulisho Kwa wepesi Kwa wananchi ambao wamevuna mazao yao na wanapeleka kwenye Maghala Kwa ajili ya kuhifadhi ili kuondolea usumbufu wakulima wanaokusudia kuhifadhi chakukula Kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Aidha Mhe.Mkuu wa Wilaya amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Mpegere kwa jitihada za uchangiaji wa Tsh. Milioni 16 na laki 2 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa Shule ya Msingi Mpegere, pia Mhe; Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi Myendaji wa Wilaya ya Kyela kupeleka Tsh, Million 5 kutoka mfuko wa Kokoa kuunga mkono juhudi hizo za Wananchi kwenye ujenzi huo wa Shule Mpya.
Kuelekea katika kipindi cha uchaguzi Mkuu Mhe.Mkuu wa Wilaya amewataka Wananchi wa Mpegere kudumisha amani na upendo,kujiepusha na vitendo vya Rushwa ili waweze kuchagua viongozi bora watakaoweza kuwaongoza na kutatua changamoto zao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa