Haya yamezungumzwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Kyela, ndugu Lucas Nyanda, alipokuwa akikabidhi ahadi ya kuchangia miradi ya maendeleo jana tarehe 26/05/202, katika shule ya msingi Nkuyu iliyopo katika kata ya Nkuyu na shule ya sekondari Nyasa lakeshore, iliyopo kata ya Matema wilayani hapa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko 60 ya saruji, ikiwa ni mchango wa Chama Cha Mapinduzi wilayani hapa amesema, chama makini hujali mahitaji ya wananchi wake, Hata ilani ya chama inazungumza swala la kuchangia maendeleo ya Nchi, hivyo kwa kutoa mchango huu ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama. Na alisema waliahidi na kukamilisha ahadi yao, na watarudi tena kutoa ahadi nyingine ili waje watamize tena, Pia lengo ni kuwahamasisha wananchi ili waige mfano wa chama chao kwa kuchangia maendeleo ya Nchi.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna, alitoa pongezi kwa chama, wananchi pamoja na kampuni ya Bioland ambao kwa pamoja wameungana katika kuchangia maendeleo katika wilaya ya Kyela. Zaidi ya mdarasa 800 yamejengwa na kukarabatiwa ikiwa ni nguvu za wananchi, serikali pamoja na wadau wa maendeleo kama, kampuni ya Bioland na mshirika wake Kim's "chocolate".
Aidha Diwani wa kata ya Matema iliyopo hapa wilayani Kyela Mhe. Issa Solomon alishukuru kwa msaada huo nakusema, madarasa haya yakikamilika ni faida kwa wilaya ya Kyela pia ni faida kwa wananchi wote wa Tanzania.
Mwisho katibu mwenezi wa CCM, ndugu Emmanuel Mwamlinge, aliwataka wananchi kuzidi kukiamini chama chao, kwani Chama Cha Mapinduzi ni chama ambacho kipo kwa ajiri ya utatuzi wa matatizo pamoja na maendeleo ya Taifa.
Ujenzi wa Vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari Nyasa lakeshore, iliyopo kata ya Matema wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa