Mtaalamu wa TEHAMA, kutoka Tume Huru ya Uchaguzi, akionyesha kwa vitendo jinsi mfumo wa kuboresha taarifa za mwananchi katika daftari la mpiga kura, zoezi lililofanyika leo tarehe 15/06/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Tume Huru ya Uchaguzi imekutana na kufanya kikao na Maafisa Mwasiliano wa Mikoa na wilaya zote Tanzani ili kupeana elimu juu ya uendeshaji wa zoezi la kuboresha taarifa katika daftari la mpiga kura.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao, Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, Ndugu Ramadhani Kailima amesema;
Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania, inawategemea sana Maafisa Habari katika kutoa elimu ya zoezi la uboreshaji wa taarifa katika daftari la mpiga kura, pia kutoa habari na kuwatangazia wananchi ili waweze kujua zoezi lote la uboreshaji wa daftari la mpiga kura.
Aidha amesema lengo la kukutana katika kikao hiki, ni pamoja na kujulishana mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya uboreshaji wa daftari la mpiga kura.
Amesema tume itafanya uzinduzi wa daftari la mpiga kura tarehe 01/07/2024 katika mkoa wa Kigoma.
Na Waziri wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa atakuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Pamoja na hayo amesema, Tume imejipanga katika kutoa elimu kila eneo, kila kundi, ili kuhamasisha wananchi kujitokeza katika kufanya maboresho ya taarifa katika daftari la mpiga kura.
Kauli Mbiu:
"KUJIANDISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA".
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa