Halmashauri ya wilaya ya Kyela inatarajia kutoa ajira za mda mfupi kwa kaya maskini kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF).
Haya yamezungumzwa na Afisa ufuatiliaji na usimamizi wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) Ndugu. Hamisi Mtoni Majani wilayani hapa, alipokuwa katika ziara yake ya usimamizi wa ugawaji wa fedha kwa kaya maskini.
Ajira hizi zitaanza kutolewa mwaka huu na zitalenga wananchi wote wanahudumiwa na mpango wa kunusuru kaya maskini yaani TASAF.
Aidha amesema katika awamu ya tatu mzunguko wa 17 wa mpango huu bado kumekwa na mafanikiao makubwa sana yakuwafikia wananchi wanaoishi katika mazingira duni ya kimaisha.
Kwani tangu kuanza kwa mpango huu wa kunusuru kaya maskini hadi sasa TASAF imefanikiwa kuzifikia kaya 4829 katika Wilaya ya Kyela.
Aliendelea kueleza siri ya mafanikio haya makubwa Kuwa, ni ushirikiano mzuri kati ya ngazi za juu za uongozi hadi ngazi za chini.
Aidha alitoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Kyela kwa kuweka utaratibu mzuri wa upatikanaji wa fedha za TASAF kwa wakati.
Katika Wilaya ya Kyela TASAF imekuwa na ruzuku za aina kuu mbili, ruzuku ya kwanza ni ruzuku ya msingi na ruzuku ya pili ni kutoa ruzuku ya masharti kwa kaya husika.
Aidha ruzuku ya msingi imejikita katika uongezaji wa kipato kwa kaya maskini pamoja na kuwezesha rasilimali watu kwa kuwaunga katika asasi mbalimbali za kifedha ili waweze kujipatia mikopo.
Ruzuku ya masharti kwa kaya maskini hii imejikita katika kutoa elimu na maswala ya kiafya ikiwemo kuwaunga walengwa katika mfuko wa Bima ya Afya CHF.
Kwa upande wao wananufaika, wamesifia mpango huu wa kunusulu kaya maskini wilayani Kyela, kwani kwa kupitia mpango huu baadhi ya kaya maskini wameweza kujipatia mitaji mbalimbali ikiwemo, mitaji ya kufanya biashara ndogondogo, Kilimo na hata kukubalika kukopa katika vikundi mbalimbali vya kifedha.
Bi. Fatuma Hassan Maulid ni mmoja wa wanufaika wa mpango huu "nimeweza kuwasomesha wajukuu wa 4 mmoja akiwa Kidato cha nne, cha tatu ,na wajukuu wawili bado wapo shule ya msingi, naishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuimalisha mpango huu Mungu aibariki Serikali yetu" alisema.
Aidha wanufaika wengine wa mpango huu wa kunusuru kaya maskini,wameipongeza serikali ya awamu ya tano, na kuiomba Serikali kutositisha mpango huu, kwani mpango huu umeweza kuondoa watoto wa mitaani na kutokomeza biashara ya ukahaba wilayani hapa.
Mwisho Mtendaji wa kijiji cha Ikombe wilayani Kyela ndugu. John Haule aliipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kusaidia kaya maskini 123 katika kijiji chake, ambapo kaya hizo zimeweza kujikwamua katoka katika hali ya umaskini, sababu kuna baadhi ya kaya wamefuga, wamejenga nyumba na hata kusomesha.
Bi.Fatuma Hassan Maulidi aliweza kusomesha wajukuu wa nne kwa fedha za kunusuru kaya masikini (TASAF).Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini wakichukua mgao wao leo wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa