Haya yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Ndugu Ezekiel Magehema alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea vituo vya zahanati vya hapa wilayani, ziara aliyoianza tarehe 03/02/2020.
Amesema, anafanya ziara katika zahati zote atazoweza kutembelea yaani zahanati ambazo zimekamilika na ambazo hazijakamilika ili kujua matatizo yake kwa kuona, ili wanapopata fedha waweze kuzisaidia zahanati hizo hata kwa asilimia 50 kwa kuanzia.
Pia Mkurugenzi Mtendaji ndugu Ezekiel Magehema amesema, serikali imeleta shilingi milioni 200 katika zahanati ya Kilasilo, ili ziweze kufanya kazi ya kuipanua zahanati hiyo na kuwa kituo cha Afya.
Akipita katika zahanati inayojengwa katika kijiji cha Isaki kata ya Katumba wilayani hapa, Mkurugenzi amewataka watendaji wa kijiji na mwenyekiti wa kijiji, kukazana kuwahimiza wanakijiji kuongeza kasi ya ujenzi wa zahanati yao kwani bati zipo ambazo zimetolewa na bandari. Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji hicho alitoa shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji kwani yeye amekuwa ni kiongozi wa pili kufika katika kijiji hicho tangu uhuru.
Mkurugenzi Mtendaji Ezekiel Magehema(mwenye suti nyeusi) akiwa katika ujenzi wa zahanati ya Isaki kijiji cha Isaki kata ya Katumbasongwe wilayani hapa.
Akiwa katika ziara hiyo ndugu magehema alifanya ziara ya kushtukiza katika shule ya sekondari ya Katumbasongwe, ambapo aliwakuta walimu wakiendelea na kazi za ufundishajimadarasani,na alitoa pongezi kwa kazi nzuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela amepanga kufanya ziara mbalimbali ikiwemo ziara ya kutembelea shule za msingi na sekondari baada ya kumaliza ziara katika Idara ya Afya.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa