Haya yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Ndugu Ezekiel Magehema alipokuwa akifungua kikao cha kamati ya Lishe ya wilaya ya Kyela, leo tarehe 18/12/2019 hapa wilayani Kyela.
Amesema, kamati ya lishe ni moja kati ya kamati muhimu sana na ni kamati mama, hivyo amewataka wajumbe wa kamati kujadili ambayo yatakwenda kuwasaidia wananchi wengi.
Aidha amesema, ili wananchi waweze kufanyakazi kwa uhakika na kutimiza ndoto zao za maendeleo, wanahitaji afya bora ambayo inapatikana kwa chakula bora. Pia alitoa ushauri kwa wanakamati kwamba, ni vizuri kukaa na watendaji wa Kata na Vijiji ili kuwaelekeza kuwa, waifanye ajenda ya lishe kuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyao vyote.
Kikao cha kamati ya lishe cha wilaya, kimefanyika leo kwa lengo la kujadili maswala ya lishe katika jamii ya wana Kyela, ili kupata njia mbalimbali za kuhakikisha wilaya inakuwa na kizazi chenye afya bora.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa