Haya yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono, alipokuwa akifungua baraza la robo ya 4 la Waheshimiwa Madiwani, katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 30/08/2022.
Mheshimiwa Mwenyekiti amesema, Halmashauri imetenga kiasi cha sh.milioni 20 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Orofea lililoko Mamlaka ya Mji mdogo wa Wilaya ya Kyela. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Katule Kingamkono alisema, fedha hizo zimetolewa kwenye mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Aliendelea kwa kusema soko litakalokarabatiwa litasaidia kukidhi mahitaji ya wananchi wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Kyela mbao wanakosa mahitaji muhimu ndani ya soko la sasa.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Ndugu Ezekiel Magehema alisema ukarabati wa soko hilo utakamilika ndani ya muda ili lianze kutoa huduma.
Alisema atahakikisha soko hilo linakarabatiwa katika viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa.
Aidha alilipongeza baraza la madiwani kwa kuibua ujenzi wa miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi.
Kwa sasa ujenzi wa miradi inayoendelea ni kama ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela pamoja na vituo vya Afya vinne ambavyo ujenzi wake umekamilika na vingine vinatoa huduma za matibabu.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa