Mheshimiwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Katule G.Kingamkono akikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Nduka.
Haya yamezungumzwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono alipowatembelea wananchi wa kata ya Ngana katika kitongoji cha Nduka tarehe 19/11/2021.
Akizungumza na wakazi hao katika kitongoji cha Nduka, Mheshimiwa mwenyekiti amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao hasa katika suala la elimu, amesema shule ya msingi Nduka hajafanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2021, hii inatokana na wazazi kutothamini suala la elimu kwa watoto wao.
Aidha amesema,
Kitongoji hichi kipo mbali sana kutoka makao makuu ya wilaya, ila serikali bado inaikumbuka Nduka ndio maana ilileta shilingi 25,123,000/= kwa ujenzi wa nyumba ya mwalimu Mkuu na bado ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa unaendelea.
Vyumba 2 kati ya 5 vinavyoendelea kujengwa katika shule ya msingi Nduka.
Pia Mheshimiwa mwenyekiti wa halmashauri aliwaasa wananchi wa Nduka kusimamia eneo la kilimo cha michikichi, Pia aliwaahidi kuwaletea miche 600 ya michikichi kutoka halmashauri. Alisema kwa kila kaya itatakiwa kupanda miche 10 na itakayobakia ipandwe katika mashamba mbalimbali,Ili itakapoanza kuzaa iwasaidie katika kujikimu kimaisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti akianza safari ya kutembea kwa mguu umbali wa zaidi ya kilomita 15 ili kujua maisha harisi ya wananchi wa Nduka.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Katule alisema kwa sasa macho yote yanaelekezwa Nduka ili kuwaletea maendeleo yenye tija ili baadae viongozi wa Nchi wapitikane kutoka Nduka. Alisema ikifanikiwa Nduka basi hata Nchi yetu itakuwa imefanikiwa.
Mheshimiwa Katule G. Kingamkono akiwaaga baadhi ya viongozi wa Nduka waliomsindikiza na waliofika kumpokea baada ya kutembea kwa masaa zaidi ya 2 na nusu kwa mguu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa