Haya yamezungumzwa na Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Claudia U. Kitta, alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la Waheshimiwa madiwani, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, tarehe 01/04/2020.
Akizungumza na viongozi pamoja na wananchi waliohudhiria kikao hicho amesema, sio vizuri kwa wazazi ambao wanawaachia watoto wao kwenda kuzurula na kukutana na makundi mtaani, kwani nia ya serikali kufunga shule, ni pamoja na kuwataka wanafunzi kutulia majumbani wakiwa na wazazi wao. Hii ikiwa na lengo la kuwaepusha watoto na maambukizi ya ugonjwa hatari wa CORONA CIVID 19. Ili jambo la kufunga shule liwe na maana, ni vizuri kuwazuia watoto wetu wasiweze kukutana na makundi ya watu ikiwa ni njia ya kujiepusha na gonjwa hili la hatari.
Aidha Mkuu wa wilaya amewaagiza viongozi kwenda katika kata na vijiji vyao, kukataza tabia ya kukaa na msiba kwa mda mrefu kwani yaweza kuleta maambukizo ya ugonjwa wa CORONA, hivyo amewataka wananchi wowote watakaopatwa na msiba, wajitahidi kufanya mazishi mida ya asubuhi ili kupunguza makundi katika msiba.
Pamoja na hayo Mhe. Mkuu wa wilaya amewatoa hofu, wananchi wa wilaya ya Kyela kwa kusumbuliwa na tatizo la maji. Amesema hadi sasa serikali yao ya awamu ya tano, imeshaleta vifaa vingi sana vya maji, hii ikiwa ni maandalizi ya uchimbaji wa kisima kirefu cha maji, ambacho kitasaidia kupunguza tatizo la maji katika wilaya ya Kyela.
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Hunter Mwakifuna, aliwataka wafanyakazi wa Kyela kuishi kwa amani na kupendana na kuheshimiana, ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi wa Kyela na Tanzania.
Pamoja na hayo Mhe. Hunter hakusita kutoa pongezi kwa shirika la umeme TANESCO, kwa kupunguza adha ya kukatika kwa umeme kila wakati, sababu kila umeme unapokatika shirika hili kwa sasa limekuwa likirekebisha hitirafu ya umeme kwa haraka zaidi ukilinganisha na siku za nyuma.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa