Afisa maendeleo ya Jamii Ndg. Victor Kabuje ameongoza Mafunzo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu waliopata Mikopo ya 10% iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 7/2/2025.
Akitoa mafunzo hayo Afisa maendeleo ya Jamii Ndg.Victor Kabuje amewataka wote waliobahatika kupata mikopo hiyo kwa awamu ya Pili kuwa na mtazamo chanya juu ya Mikopo hiyo ili iweze kuwanufaisha katika maisha yao.
Ndg. Kabuje amevisihi Vikundi hivyo kuwa na nidhamu ya pesa,Uaminifu na kuweka akiba ya Fedha kupitia vyanzo vyao vya Mapato.
Aidha Kabuje amewaomba Wafanyabiashara pamoja na Wajasiriamali hao kufuatilia Vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii ili kupata fursa na kujifunza njia mbalimbali zitakazoweza kuwasaidia kuboresha na kukuza biashara zao.
Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kyela Bi. Judith Mashasi amewasihi waliopata Mkopo huo kutumia na kurejesha kwa wakati Fedha hizo ili kuepukana na makosa 34 ya Rushwa ikiwemo kutumia vibaya Fedha za Serikali.
Vilevile Bi. Judith Mashasi amevitaka Vikundi vyote vilivyopata Mkopo kuwa na ushirikiano mzuri utakaowasaidia kuendeasha Biashara zao na kuweza kujikwamua Kiuchumi.
Bi. Judith amesisitiza kuwa Serikali inatamani kuona Mikopo hiyo ikileta mabadiliko chanya kwa wanufaika, huku akiwahimiza kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta maendeleo endelevu
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa