Viongozi mbalimbali kutoka nchi ya Malawi wamefika wilayani Kyela kwa lengo la kujifunza njia za ukusanyaji wa mapato.
Elimu hiyo imetolewa chini ya Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Adamu Kabeta tarehe 04/09/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri.
Waliohudhurua semina hiyo ni pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nchini Malawi, ikiwemo Mkuu wa wilaya ya Kalonga Mhe. Frank Mkandawile, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wataalam kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Akizungumza katika zoezi hilo Katibu tawala (w) Bi. Sabrina Houmud amesema Elimu hiyo itakua chachu ya kubadilishana mawazo baina ya Nchi ya Malawi na Tanzania husani wilaya ya Kyela, kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Kalonga Mhe. Frank Mkandawile, ameishukuru Halmshauri ya wilaya ya Kyela, kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili, hadi kufikia hatua ya kutoa kubadilishana uzoefu wa kujua mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Kyela, Mhe. Adam kabeta ameishukuru serikali ya Malawi, kwa ujio wao Tanzania kwa lengo la kupata elimu katika wilaya ya Kyela, kwani kupitia elimu hiyo itasaidia kukuza uchumi, umoja na mshikamano baina ya nchi ya Tanzania na Malawi.
Wakiwa katika mafunzo hayo, baadhi ya madiwani nchini Malawi walipata fursa ya kuuliza maswali ikiwa ni pamoja na suala ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara, wakulima na leseni kwa wavuvi wa ziwa nyasa, ikiawa na utunzaji wa mazingira.
Akijibu swali la ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara, Mkuu wa kitengo cha Fedha wilayani Kyela, CPA. Agustino Manda amesema, idara husika, kikiwemo kitengo chake, hushughulikia ukusanyaji wa mapato kwa maana ndio wenye ufahamu juu ya elimu ya mapato, kwa upande wa wakulima amesema, mkulima mkubwa anapaswa kulipia ushuru pia.
Katika suala la leseni kwa wavuvi wa ziwa Nyasa, Afisa kilimo Ndg. Pantaleo Mushi amesema kwa sheria ya nchi ya Tanzania suala la leseni kwa wavuvi ni muhimu kwani inamuwezesha mvuvi kufanya shughuli zake pasipo na usumbufu.
Vilevile Afisa mazingira Ndg. Daule Husein ameeleza njia tunayoitumia katika utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kampeni ya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, pamoja na vifaa tunavyotumia kukusanya uchafu katika mazingira maeneo tofauti.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa