Vitabu 44674 imegawiwa katika shule za msingi Kyela, vitabu ambavyo vimegawiwa na Kampuni ya Bioland kupitia mradi wa kokoa for schools unaotekelezwa katika Halmashauri 3 ikiwemo Halmashauri ya Kyela, Rungwe na Busokelo.
Kampuni ya Bioland kupitia mradi wa kokoa for schools inayojishughulisha na ununuzi wa zao la Kakao mpaka mwaka 2022 imejenga jumla ya vyumba 805, kukarabati vyumba 826 pamoja na ujenzi wa Hostel ya wanafunzi wa kike kwa Halmashauri ya Kyela na Busokelo.
Akikabidhi vitabu hivyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Fons Maex amesema kampuni hiyo inafanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhira zake kwa wananchi walimao kokoa katika ukanda wa halmashauri hizi 3 na anafanya hivi mara tu baada ya kupata faida.
Aidha Bwana Maex ameeleza kuwa msaada huo wa vitabu utaenda kuongeza kiwango Cha ufaulu shuleni huku akiahidi kuwa Mwalimu atakayefaulisha kiwango Cha daraja A kwa kila mwanafunzi atapewa motisha ya shilingi 10,000/= .
Ameongeza kwa kusema kampuni ipo Mbioni kuanzisha Tuzo maalumu kwa shule zitakazofanya vizuri (Cocoa for schools awards) ambapo shule itakayofanya vizuri itapewa kiwango Cha shilingi 500,000/= ya pili 25,000/= na tatu 125,000/=.
Akiongea na walimu waliokuja kuchukua vitabu hivyo Mhe. Ally Mlaghila Jumbe (MB) amesema, Mtu kwanza anaestahili sifa ni mwalimu, kwa sababu mwalimu ndie anaetengeneza tabia ya watoto tangu wakiwa wadogo hadi wanakuwa.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Mbunge alisema Phons yupo hapa Kyela, kwa sababu ameipenda sana Kyela. Aliendelea kusema kwamba Mr. Phons ametoa bilioni 13 kwa ajiri ya wilaya Kyela. Na hata hivyo alisema wanaKyela bado hatujamtumia vizuri mdau huyu, Hivyo aliwaomba walimu kutukomboa kifikra ili tuweze kufaidika zaidi na mdau huyu.
"Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 8 kwa ajiri ya mradi mkubwa wa maji wa Ngana group mradi utakaotoa huduma kwa wilaya ya Kyela" amesema Mhe. Mbubge. Hivyo hatunabudi kuwaheshimu viongozi kama hawa ambao wanaruhusu wadau kama hawa kuisaidia nchi yetu kwa maendeleo kama afanyavyo kiongozi wetu wa nchi.
Mwisho aliwashukuru wadau wa kokoa for schools kwa msaada wao mkubwa katika wilaya ya Kyela.
Wakati huo huo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (W) Mhe. Gervas Ndaki amesema, Mwalimu wa shule ya msingi ni mlezi wa watoto kwa sababu anawapokea watoto na kuwalea. Alisema pamoja na yote ambayo yanafanywa na wadau hawa, aliwaomba wadau wa kokoa for school kuongeza motisha kwa walimu wa shule za msingi kwani walimu hawa wanafanya kazi kubwa sana.
Pia alitoa shukrani zake nyingi kwa wadau hawa kwa msaada wa vitabu ambavyo vimetolewa kwa shule za msingi. Na alitoa shukrani kwa Mhe. Mbunge Ally Mlaghila Jumbe kwa kuzidi kukaa karibu na Mr. Phons ili kutatua changamoto ndogondogo zinazojitokeza juu yake na kuzimaliza.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Ezekiel H. Magehema mesema,
Ikiwa kama madarasa yapo na madawati yapo na Mkuu wa shule yupo na akiwa ni kiongozi mzuri kwa vyovyote vile shule hiyo itafanya vizuri. Amesema anawashukuru sana wadau wa cocoa for schools, kwa kutoa vitabu vya Hesabu na kingereza kwa darasa la 4 na darasa la 7 pia alishukuru kwa ahadi nzuri ya kuanzia mpango wa kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
kwani mpango huu ni mwema na ni njia nzuri ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuinua kiwango cha elimu katika nchi yetu ya Tanzania.
Mwisho amewaomba wadau hao kutusaidia katika ujenzi wa vyoo na mabweni katika shule zetu, ingawa kuna baadhi ya shule tayari wamesha jenga mabweni.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa