Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase, amefanya kikao cha waganga wa tiba asili, jadi na vyombo vya habari, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 28/6/2024.
Akizungumza na waganga wa tiba asili na jadi Mhe. Mkuu wa wilaya amesema, serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa waganga wa tiba asili na jadi katika jamii, hivyo amewaomba kuwa na ushirikiano na viongozi wa serikali, ili wafanye kazi kwa kufuata sheria na miongozo waliojiwekea.
Mhe. Mkuu wa wilaya amekemea mila chonganishi, vitendo vya ukatili kwa baadhi ya waganga wa tiba asili na jadi kuwadanganya wateja wao kuwa viungo vya binadamu vinaleta nyota au vinaleta utajiri.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya ameomba viongozi wa chama cha waganga wa tiba asili na jadi kuwasisitiza wanachama wao kufuata sheria na utaratibu wa kupata vibali na barua kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri, vibali vitakavyowawezesha kutambulika rasmi na serikali.
Vilevile Mhe. Mkuu wa wilaya amewataka Watendaji wa kata na viongozi wa vijiji, kuwa na orodha maalumu ya waganga wa tiba za asili na jadi, pia kujua mahali wanaopatikana katika kata zao ili kutoa huduma halali kwa wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa