Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Kyela Mhe.Katule G.Kingamkono ameongoza Baraza la robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024-2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 29.5 2025
Akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya,Katibu Tawala Wilaya ya Kyela Bi.Sabrina Hamoud amewapongeza Wah.Madiwani kwa ushirikiano na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupia wataalamu wake kwa ukusanyaji wa mapato uliopelekea kununua mtambo mkubwa wa kutengenezea barabara.
Awali Mhe.Katule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha miradi ya maendeleo inaanzishwa na kukamilika kwa wakati.
Aidha Mhe.Mwenyekiti amewapongeza Madiwani kwa kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato kwenye kata kwani hapo awali Halmashauri ilikua ikikusanya Tsh.bilion 2.7 lakini mpaka sasa Halmashauri imeweza kukusanya mapato hadi kufikia Tsh.bilioni 8.1
Mhe.Katule ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha amani na Usalama vinapatikana ,pia ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na wataalamu kuanzia ngazi ya Kata kwa ushirikiano mzuri katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia Wananchi.
Sambamba na hayo Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri amewapongeza na kuwaomba Wataalamu kufanya juhudi katika zoezi la ukusanyaji wa mapato,kwani kupitia mapato hayo Halmashauri iliweza kununua mtambo wa kutengeneza barabara,pia mapato hayo yatasaidia kununua mitambo mingine kama Roller, Grader zitakazowasaidia kutatua changamoto ya miundombinu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa