Waheshimiwa Madiwani wilaya ya Kyela, wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo Inayotekelezwa wilayani tarehe 25.04.2024.
Ziara hiyo imejumuisha, Kamati ya Elimu na Afya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu, Victor Kabuje akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wametembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Itenya kata ya Ngonga wenye gharama wa Tsh. Milioni 40, Ukarabati wa chumba cha watoto wachanga (NICU) Pamoja na kibanda cha Kupumzikia ndugu wa Wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela, wenye thamani ya Tsh. Milioni 35, pamoja na Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi, wenye uhitaji maalum katika Shule ya msingi Sama kata ya Ibanda wenye thamani ya Tsh. Milioni 128.
Pamoja na hayo, waheshimiwa Madiwani wamepongeza mwenendo mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika kata mbalimbali wilayani Kyela.
Nae makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Adam Kabeta Amewaasa viongozi na wasimamizi wa miradi kuwashirikisha wananchi katika miradi inayoletwa katika jamii, ili waendelee kujionea juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa