Madiwani kutoka Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro wamefanya ziara tarehe 24.05.2024 wilayani Kyela, kwa lengo la kujifunza ukusanyaji wa mapato pamoja na uzalishaji wa zao la kakao katika Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
2023/2024 Halmashauri ya wilaya ya Kyela makisio ya bajeti yalikua ni bil 4.8 lakini makusanyo halisi hadi mwezi Mei 2024 ni zaidi ya bil 5 sawa na asilimia 109, ambapo zao la kakao limechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
Madiwani hao kutoka wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, wamepata fursa ya kujifunza kuhusu usindikaji wa zao la kakao hatua hatua mpaka kufikia hatua ya mauzo.
Akizungumza na Waheshimiwa hao, Kaimu Afisa Kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Ndugu Pantaleo Mushi, amewaelekeza hatua kwa hatua katika uandaaji wa vitalu vya miche ya kakao na vitu muhimu vinavyohitajika katika uzalishaji wa miche hiyo.
Mwisho Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi Ndugu Gasto Silayo, amewashukuru viongozi na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela kwa mapokezi mazuri.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa