Waheshimiwa Madiwani kutoka wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wametembelea halmashauri ya wila ya Kyela leo tarehe 19/12/2023, kwa lengo la kujifunza jinsi ya kulima zao la kakao.
Waheshimiwa madiwani 20 wakiwa wameambatana na wataalam wa kilimo kutoka halmashauri ya Mvomero wameongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa baraza la madiwani la Mvomero, Mhe. Christopher John Maarifa, na kupokelewa na wenyeji wao ambao ni baadhi ya madiwani na wakuu wa Idara na Vitengo, wa halmashauri ya wilaya ya Kyela, wakiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Katule kingamkono.
Katika ziara yao waheshimiwa Madiwani wametembelea kitalu cha miche ya miti ya kakao, kilichopo kata ya Bondeni, AMCOS ya Mali Hai iliyopo kata ya Nkuyu ili kujifunza ukusanyaji wa zao la kakao, wametembelea kituo cha kuvundika kakao katika kata ya mababu "Mababu CCF" pamoja na eneo la utalii katika fukwe za ziwa Nyasa.
Aidha Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero wametoa shukrani kwa elimu nzuri waliyoipata ya kilimo cha kakao pia mapokezi mazuri na kuahidi kwenda kuhamasisha ulimaji wa zao hilo kwa wingi katika wilaya yao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa