Waheshimiwa Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kyela wakiwa wanapata utambulisho mfupi tayari kwa maandalizi ya kutembelea miradi Mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji katika halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Kyela wamefanya ziara ya siku nne katika Mkoa wa Songwe na Mkoa wa Mbeya ziara iliyoanza tarehe 21/12/2021 na itamalizika tarehe 24/12/202.
Hii ni ziara ya kawaida ambayo viongozi wa serikali hufanya kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ili kuboresha huduma na maendeleo katika maeneo yao ya utawala wanayotoka.
Hadi kufikia tarehe 22/12/2021, Waheshimiwa Madiwani wameweza kutembelea mradi wa mashine ya ufyatuaji wa matofali ya saruji, mradi wa maegesho ya magari, mradi wa ujenzi wa shule ya mchepuo wa kingereza, mradi wa duka la dawa, soko la mazao haya yote ni katika wilaya ya mji wa Tunduma mkoani Songwe.
Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Kyela wakiwa wameingia katika moja ya stendi ya maegesho ya magari, ikiwa ni moja ya chanzo cha mapato katika halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameweza kukutana na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini, Mheshimiwa Mwalingo Kisemba pamoja na wakuu wa Idara wa halmashauri hiyo lengo ikiwa ni kubalishana mawazo juu ya utawala bora, unaojumuisha masuala ya Utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria, haki na usawa kwa watu wote.
Pamoja na hayo, Waheshimiwa Madiwani wameweza kujifunza kuhusiana na njia mbalimbali za ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya Mbeya vijijini,na kupata fulsa ya kutembelea mradi wa mashine ya ufyatuaji wa matofali ya saruji na mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri hiyo. Ziara bado inaendelea.
Waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Kyela wakipata maelekezo katika moja ya mradi wa ufyatuaji wa matofali ya saruji (Block) katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa