BARAZA la madiwani wa halmashauri ya wilaya Kyela, limetakiwa kuwahamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi, kuboresha taarifa zao katika daftari la wapiga kura, wanapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Imeelezwa, wafanye hivyo wakati utakapofika ili kuhakikisha wananchi wanaboresha taarifa zao katika daftari hilo, lakini pia anawaomba uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba mwaka huu, ukapate kuwa tulivu.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya Kyela, Josephine Manase, wakati akizungumza na madiwani wa halmashauri, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Kyela.
“Na tuendele kuhakikisha kwamba tunatoa elimu, kwa wananchi wetu kuhakikisha kuwa wanashiriki katika zoezi hili, muhimu sababu tunakwenda kuchagua viongozi ambao watakwenda kutuwakilisha vyema…” alisema Mhe. Josephine.
Aliongeza viongozi hao watakwenda kupokea kero zao, na kwenda kuzisemea sehemu sahihi, hivyo waendelee kutoa elimu kwa wananchi, kwani kuna wengine wanaweza kuona uchaguzi huo wa serikali za mitaa siyo muhimu.
“Uchaguzi huu ni muhimu sababu wale viongozi wa serikali za mitaa, tunaokwenda kuwachagua ndiyo watakaokwenda kutusemea sisi kero zetu na changamoto zetu” alisema Mhe. Josephine.
Mhe. Mkuu wa wilaya amesema hiyo ni sehemu ambayo kila mwananchi ambaye amefikisha umri sahihi, anatakiwa ashiriki kuchagua kiongozi ambaye yeye anamuona atamuwakilisha vyema.
Mhe. Mkuu wa wilaya amewaomba madiwani wa halmashauri, kama wawakilishi wa wananchi waendelee kushirikiana, kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuboresha taarifa zao katika daftari la wapiga kura.
“Lakini pia utakapofika muda wa uchaguzi, basi washiriki katika zoezi hilo la upigaji kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa” alisema Josephine.
Hata hivyo Mhe. Manase amewaomba wananchi kujitokeza katika kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye anatarajia kufanya ziara katika wilaya yetu siku ya jumapili tarehe 12/01/2024 kuanzia saa 01:00 Asubuhi.
Mwisho…
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa