Waheshimiwa Madaiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wapewa elimu kuhusiana na Mfumo wa kukusanyia mapato Tausi.
Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 18/10/2023 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya.
Lengo la kujifunza mfumo huo wa Tausi ni pamoja na kutaka kuufahamu Mfumo na kusaidia kuusimamia ili kuonheza Mapato katika wilaya Kyela.
Mfumo wa Tausi ni mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato, kwenye serikali za mitaa.
Lengo la kuanzisha huu mfumo ni kutatua, changamoto zilizokuwa zina jitokeza kwenye mfumo wa zamani wa ukusaji wa mapato LGRCIS.
Jina la mfumo limetokana na aina ya ndege wa Tausi walioko Ikulu kwa hivyo jina la TAUSI halina kirefu chake.
Kyela ni yetu kwa pamoja tutaijenga na kuilinda wilaya yetu.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa