Haya yamejiri wakati Waheshimiwa Madiwani wilaya ya Kyela wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa ziara za kutembelea na kukagua miradi kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 05/03 hadi 07/03/2024, ikijumuisha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Kamati ya Elimu na Afya, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Pamoja na wataalamu kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani na wataalamu wametembelea Mradi wa ujenzi wa kichomea taka na ujenzi wa mnara wa kupandishia maji katika zahanati ya Ngyeke Tsh. 62,474,500/= (SRWSSP), mradi wa umwagiliaji wa skimu ya Makwale wenye thamani ya zaidi ya bilioni 20, Ujenzi wa kituo cha afya Makwale, mradi wa ujenzi wa matundu 22 ya vyoo katika shule ya msingi Mbogela wenye thamani ya shilingi 58,089.815 (SRWSS).
Ujenzi wa shule Mpya ya Wasichana ya Mkoa kata ya Busale yenye thamani ya shilingi 3,000,000,000/= Kutembela mashine yakukoboa mpunga katika kijiji cha mbako kata ya Ikimba wenye thamani ya Tsh. 47,500,000/=(DADPs).
Ujenzi wa vyoo, tanki la kuvuna maji ya mvua, kichomea taka, ukarabati wa choo katika chumba cha wazazi, mnara wa kupandishia maji katika zahanati ya kandete.
Pamoja na miradi hiyo, Miradi mingine iliyotembelewa na kaguliwa ni mradi wa shamba la mkulima la michiki ambapo ni matunda ya kugawa bure miche kutoka halmashauri, kutembelea shamba la mkulima wa kakao kata ya Ndandalo, ujenzi wa ofisi ya kata, ukarabati wa jengo la zahanati ya njugilo, ujenzi wa zahanati ya Malangali miradi yote kutoka katika kata ya Ipande, Ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Lubele, ujenzi wa maabara katika kituo cha afya Ngonga.
Miradi yote iliyotembelewa na kukaguliwa imeridhiwa na waheshimiwa madiwani ikiwa ni pamoja na kutoa baadhi ya maoni kwa marekebisho, pongezi na kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta fedha nyingi zinazotekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya Kyela.
Aidha waheshimiwa madiwani wametoa maagizo ikiwemo agizo la umaliziaji wa miradi ya maendeleo kwa ubora na kuzingatia muda uliopangwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa