Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, Katibu Tawala wilaya Bi. Sabrina Hamoud amesema;
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ametoa shukrani kwa Waheshimiwa madiwani kwa kuanzisha mfuko wa kuwasaidia wazee kupata bima ya Afya (iCHF), ambapo amesema ataongea na Mhe. Mkuu wa Mkoa ili kuanhalia uwezekano wa kupata fedha kutoka Idara ya afya ili kuona ili kuongeza katika mfuko ulioanzishwa kuajili ya kuwasaidia wazee.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya ametoa shukrani kwa wananchi ambao walijitolea mashine za kupasua mbao ambazo zimesaidia utengenezaji wa madawati katika shule zilizopo wilayani Kyela, ambapo mbao 270 zilipokelewa na uongozi wa wilaya.
Vilevile amesema Mhe. Mkuu wa wilaya amepongeza umoja uliopo baina ya viongozi wa wilaya, pia amewataka kuendelea kuitunza amani tuliyonayo, hasa tunapoelekea katika uchaguzi mdogo.
Awali Mwemyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule Kingamkono, amesema kwa sasa halmashauri imejipanga kuziba mianya yote ambayo inasababisha kutorosha mapato.
"Tusitake mtu yeyote atuchezee Kyela, haiwezekani watu wachache wanufaike wakati wengine wakiendelea kuumia" amesema Mhe. Katule.
Pia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kuwaondoa mawakala wote amabo sio waaminifu katika kukusanya mapato ya serikali.
Aidha amesema Baraza la Madiwa Kyela limeanzisha Mfuko maalumu wa kuchangia fedha, kwa ajili ya kuwasaidia wazee wasiojiweza utakaosimamimiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kyela.
“Sasa wanaKyela tunataka kuelekeza nguvu zetu katika kuwasaidia wazee wetu” alisema Kingamkono.
Mwisho alitoa pongezi kwa watumishi wote pamoja na viongozi kwa ushirikiano na uchapakazi unaoleta maendeleo ya kweli wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa