Waheshimiwa Madiwani wilaya ya Kyela, wametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani, tarehe 29-30.04.2024.
Ziara hiyo imejumuisha, Kamati ya Uchumu, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, kamati zilizoongozana na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Florah Luhala, akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Aidha kwa kupitia kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Waheshimiwa Madiwani wametembelea miradi mbalimbali ikiwemo, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Ibungu kata ya Ikimba, Ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Itunge, shamba la mkulima wa kakao kata ya Itope, pamoja na kufuatilia miti iliyopandwa katika shule ya msingi Kilambo ili kujua inavyoendelea.
Vilevile Waheshimiwa madiwani kwa kupitia Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wametembelea na kukagua miradi ya Skimu ya umwagiliaji katika kata ya Makwale, shamba la michikichi katika kata ya Itope, wamekagua Maguta yakusombea taka katika ofisi za halmashauri, Ukarabati wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya msingi Mwaya, pamoja na ukarabati wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya msingi Mababu kata ya Mababu.
Pamoja na hayo, waheshimiwa Madiwani wamepongeza mwenendo mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika kata mbalimbali wilayani Kyela.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono, Amewaasa viongozi na wasimamizi wa miradi kuwashirikisha wananchi katika miradi inayoletwa katika jamii husika.
Ili wananchi, waendelee kujionea juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, pia amewataka maafisa ugani kuanzisha vitalu vya miche ya kakao katika kata zao, ili kuleta kilimo chenye tija.
Hata hivyo waheshimiwa madiwani wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na wataalam kutoka halmashauri ya wilaya ya Kyela katika suala zima la usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa