Waheshimiwa madiwani wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kupitia kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, kamati ya Fedha Uongozi na Mipango wilayani Kyela, tarehe 25-29/07/2024.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na mradi wa kikundi cha bodaboda (NIMABO)kata ya bondeni, umaliziaji wa mradi wa zahanati Kiangala kata ya Talatala, umaliziaji wa mradi wa jengo la mama na mtoto Kapamisya kata ya mwaya, shamba la kokoa kijiji cha Kapamisya.
Miradi mingine ni ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kata ya Mwanganyanga, Zahanati ya Ndandalo, Zahanati ya Nkuyu kata ya Nkuyu, Ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Lema kata ya Busale pamoja na mradi binafsi wa "Hoteli ya Songwe safari park" kata ya Ibanda.
Waheshimiwa Madiwani kupitia kamati ya uchumi ujenzi na mazingira, kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za kuanzisha na kuendeleza miradi hiyo katika wilaya ya Kyela.
Sambamba na hilo, Waheshimiwa Madiwani wamempongeza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Bi.Flora Luhala kwa usimamizi mzuri wa fedha za miradi ya maendeleo.
Vilevile Waheshimiwa Madiwani wamewapongeza wananchi wa kijiji cha Kiangala kwa ushiriki wa ujenzi wa mradi wa zahanati ya kijiji chao, kwani kukamilika kwa zahanati hiyo ni msaada kwa kata husika na kata za jirani.
Pamoja na hayo Waheshimiwa Madiwani wamewapongeza wakulima wa zao la kokoa kijiji cha Kapamisya kwa utunzaji mzuri wa miche iliyogawiwa na halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Pia wametoa ushauri kwa wakulima, wazidi kutunza miche kwa njia ya kisasa hadi itakapoanza kutoa matunda ili waweze kupata mavuno kwa wingi.
Aidha Waheshimiwa madiwani kupitia kamati ya Fedha, wametoa maagizo kuhakikisha mradi wa zahanati ya Ndandalo kukamilisha maeneo yenye changamoto ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mwisho waheshimiwa madiwani wameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa