Kikao cha Bodi ya leseni za biashara kimefanyika leo 16/08/2023, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela.
Kikao kimehudhuriwa na wajumbe wa Bodi na kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Hassan Mwambokela, Mkurugenzi Mtendaji Bi. Frolah A. Luhala(katibu).
Lengo la kufanya kikao ni kujadiri mafanikio ya ukusanyaji wa mapato kupitia chanzo cha leseni za biashara kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Pamoja na hayo Kaimu Afisa biashara(W) ndugu Eliasi Awari amebainisha faida za leseni kwa mfanyabiashara zikiwemo;
1. Leseni ni kitambulisho kikuu cha mfanyabiashara hapa Tanzania.
2. Leseni ni moja ya nyaraka ya kisheria inayotumika na Taasisi za kifedha ili kumpa mkopo mfanyabishara.
3. Inasaidia kuanisha aina ya biashara na eneo ambalo mfanyabiashara anafanyia kazi.
4. leseni ya biashara humsaidia mfanyabiashara katika upatikanaji wa hati ya kusafiria.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa