Wakazi wa kata ya Itope wilayani Kyela, wamemuomba Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Josephine K. Manase, kuwasaidia katika kumuomba Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili aweze kuwasambazia umeme katika vitongoji vyote vya kata yao.
Maombi hayo yametolewa na wananchi wa kata hiyo tarehe 10/05/2023, wakati Mhe. Mkuu wa wilaya alipowatembelea wananchi hao, kwa lengo la kufanya mkutano wa kusikiliza kero.
Mkuu wa wilaya ya Kyela (katikati) akiwa ametembelea msingi wa mradi wa ujenzi wa zahanati katika kata ya Itope kabla ya kufanya mkutano wa hadhara.
Akizungumza na wakazi wa kata ya Itope Mkuu wa wilaya ya Kyela, amewatoa hofu wakazi wa kata ya Itope kuwa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikia kilio cha wananchi wa kipato cha chini hivyo ameongeza awamu nyingine ya kusambaza umeme wa REA.
Ambapo tathmini ya zoezi hilo inafanyika kwa maeneo yote yanayostahili kusambaziwa umeme huo, Ikiwemo kata ya Itope, hivyo wananchi wajipange katika kuingiza umeme mara baada ya mradi huo kuwafikia.
Kuhusiana na ulipaji wa fidia katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Ibanda hadi bandari ya Kiwira na Kiwira Itungi port Mhe. Josephine amesema, fidia zote zitalipwa hakuna mwananchi atakae achwa bila kulipwa, kwa sasa Serikali inaendelea na mchakato wa maandalizi ya malipo ya kila mwananchi anaestahili kulipwa fidia.
Kuhusiana na uvumi wa mborea za ruzuku kutokuwa na ubora na kupelekea kutokea kwa magonjwa katika zao la mpunga na migomba, Mhe. Mkuu wa wilaya amewatoa hofu wakazi wa kata ya Itope kwamba, Hakuna mbolea iliyochakachuliwa kwani serikali imejiridhisha na ubora wake, Pia serikali ni sikivu na itazidi kufanya uchunguzi wa magonjwa yaliyojitokeza katika zao la Mpunga na Migomba.
Aidha amewapongeza wakazi wa kata ya Itope kwa kuomba waanzishiwe soko katika kata yao, kwani maeneo wanayo yakutosha. Ambapo Suala hilo lilichukuliwa na Mheshimiwa Mkuu wa wilaya na kuwaahidi anakwenda kulifanyia kazi.
Pia alimuagiza mtendaji wa kata kuhakikisha vitongoji vyote vimesomewa taarifa ya mapato na matumizi ndani ya wiki mbili, ili kutoa haki ya mwananchi kujua mapato na matumizi ya fedha zote zinazoingia na kuchangwa ndani ya kata yao.
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine K. Manase ameendelea na ziara zake za kusikiliza kero kutoka kwa wananchi, tarehe 12/05/2023 aliweza kufika na kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Ndobo kijiji cha Isuba, na kusikiliza kero kutoka kwa wananchi wa Ndobo na baadhi ya kero zilijibiwa na nyingine zilichukuliwa kwa utekekezaji.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa