Kamati ya wataalam "CMT" ya halmashauri ya wilaya ya Kyela, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Florah A. Luhala, wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendele tarehe 22/07/2024.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya msingi Kajunjumele, Ukarabati wa maabara katika shule ya sekondari ya Katumba songwe, shamba la michikichi katika kata ya Ngana.
Umaliziaji wa zahanati kata ya Ngana kijiji cha Kasumulu, Umaliziaji wa jengo la mama na mtoto zahanati ya Kapamisya kata ya Mwaya, shamaba la kakao katika kata ya Mwaya, umaliziaji wa zahanati ya Kiangala kata ya Talatala.
Aidha katika kutembelea miradi hiyo, Mkurugenzi mtendaji amebaini mapungifu kwa wasimamizi wa karibu wa miradi wakiwemo watendaji na kamati za usimamizi wa ujenzi wa miradi, hali inayopelekea miradi kuto kamilika kwa wakati, Mfano mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa katika shule ya msingi Kajunjumele, ukarabati wa maabara katika shule ya Katumbasongwe, vifaa vyote vya umaliziaji vipo lakini shida ipo kwa wasimamizi wa karibu, hali iliyopelekea Mkurugenzi Mtendaji kuwapa siku chache za ukamilishaji wa miradi hiyo.
" Sioni sababu yoyote ya kuto kumalizia miradi, pesa zote zimelipwa, vifaa vya ujenzi vipo tatizo lipo wapi, Naomba tusilale tukamilishe miradi ili tuanze kutoa huduma kwa wananfunzi na wananchi" amesema Bi. Florah Luhala.
Aidha Wakuu wa Idara na Vitengo wametoa pongezi kwa miradi ya wananchi ikiwemo utunzaji wa miche ya kakao ambayo ilipandwa mara baada ya halmashauri kugawa miche kwa wakulima.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa