Timu ya wataalam kutoka halmashauri ya wilaya ya Kyela, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Florah A. Luhala leo 16/10/2023, imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo, ili kijiridhisha na kasi ukamilishaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa uwekaji wa taa katika soko la mikoroshoni, ukaguzi wa kivuko cha waenda kwa miguu katika kata ya Ngonga, ujenzi wa vyumba 2 na ofisi mbili katika shule ya sekondari Mwakilima iliyopo kata ya Katumbasongwe.
Pamoja na miradi hiyo miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba 1 ya walimu, yenye pande 2 za makazi, yaani nyumba itakayotumika na familia mbili mara baada ya kukamilika.
Pia wametembelea na kukagua mradi wa machinjio ya Kafundo, iliyokarabatiwa katika kata ya Ipinda, ujenzi wa kalvati katika kijiji cha Isuba kata ya Ndobo, Ukarabati wa jengo la CTC katika zahanati ya kata ya Makwale pamoja na umaliziaji wa jengo la bweni katika shule ya sekondari Nyasa lakeShore.
Ziara hii inafanyika ili kutambua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo na kuzipatia ufumbuzi, ili kukamilisha miradi kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa