Mkuu wa wa wilaya ya Kyela Mhe Josephine Manase, ametoa pongezi kubwa kwa walimu wa shule ya msingi Nyasa English Medium, kwa juhudi wanazo fanya katika kuhakikisha shule ya Msingi Nyasa inafanya vizuri katika suala la utoaji wa Elimu bora kwa wanafunzi wilayani Kyela.
Mhe. Manase ameyasema hayo tarehe 06/10/2023, katika zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya msingi katika shule ya msingi Nyasa English Medium, ikiwa ni mahafali ya tano (5) ya shule hiyo.
Akitoa hotuba yake, Mhe. Manase amewataka walimu na Wazazi kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri katika kuhakikisha watoto wanaendelea kufanya vizuri katika masomo.
Aidha Mkuu wa wilaya Mhe. Josephine Manase amewaasa wanafunzi wa shule ya msingi Nyasa English Medium, kuwa na maadili mema pia mfano wa kuigwa huko waendako.
Pamoja na hayo Mhe. Mkuu wa wilaya, amewataka walimu wa shule ya msingi kuendelea kuwa wavumilivu, kutokatishwa tamaa ama kutetereka na changamoto ndogo ndogo zinazo wakabili katika shule hiyo kwani hakuna kazi isiokuwa na changamoto.
Pamoja na hayo Mhe. Manase ameahidi kuifanyia kazi risala kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizo ndani ya uwezo wake kwani mchango wa shule ya msingi Nyasa English Medium wilayani Kyela ni mkubwa, Hasa katika kuitangaza wilaya ya Kyela Kimkoa mpaka Kitaifa kwa matokeo mazuri wanayoyapata kila mwaka.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa