Umoja wa wanaKyela waishio ndani na nje ya Nchi ya Tanzania, wamekabidhi vifaa tiba katika Kituo cha afya Ipinda "Mama delivery Kit", baiskeli 1ya mlemavu, Madawati 30 kwa kata ya Ipinda, kadi za iCHF iliyoboreshwa kwa kaya 60 zenye watu zaidi ya 300 ili kuwasaidia wananchi wenzao ambao wanaishi katika wilaya hii ya Kyela.
Msaada huo umekabidhiwa leo tarehe 28/12/2022 katika kituo vha afya Ipinda kata ya Ipinda hapa wilayani Kyela.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Kaimi Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Bi. Mariam Ngwere Mganga Mkuu wa wilaya amesema;
Kikundi cha IBASA kimekuwa kikishirikiana sana na serikali katika kuwasaidia wananchi wa hapa wilayani Kyela kwa takribani miaka 4 kwa sasa.
Aidha amewasihi wazazi waishio wilayani Kyela, kuendekea kuwaombea watoto wao hao ambao wanawaletea misaada ili wazidi kufanikiwa huko waliko na waendelee kutoa misaada kama hii kwa wenzao hapa wilayani.
Pia alizoa shukrani kwa msaada wa vifaa tiba, bima za Afya baiskeli ya mlemavu pamoja na madawati, yaliyotolewa kazikankata ya Ipinga ili kuweza kuwasaidia wanafunzi shuleni. kwa kufanya hivyo IBASA, wameweza kusaidiana na serikali katika kuwahudumia wananchi.
Pamoja na hayo, aliwaomba wana IBASA kutochoka katika kutoa misaada kwa wanaKyela waendelee na moyo huo wa kujitolea na Mungu atazidi kuwabariki.
Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi cha IBASA, Mwenyekiti wa kikundi hicho ndugu Isaya Mwakipesile Amesema, kikundi hiki ni kikundi cha watoto wote wa Kyela "Wanyakyusa" wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi ya Tanzania.
Lengo la kikundi hiki ni kutoa misaada mbalimbali kwa ndugu zao waishio Kyela, Pia aliendelea kuseama kwamba, hadi sasa wameshasaidia wananchi zaidi ya 1000 kwa kuwapatia kadi za bima ya Afya ili kuwasaidia pale wanapopata na changamoto ya Afya.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa