Shule mpya ya Sekondari Ibanda iliyojengwa katika kata ya Ibanda wilayani Kyela, yenye Madarasa 8, ofisi 2 za walimu, jengo la maktaba, Jengo la Tehama, matundu 10 ya vyoo ( wav 5, was 5) na Jengo la Utawala iliyogharimu shilingi 583,180,028/=.
Itahudumia watoto wa Kata ya Ibanda na kata jirani, kuanzia tarehe 08/01/2024.
Shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwakumbuka watoto wa kata ya Ibanda ambao wameteseka kwa miaka mingi kwenda kufuata masomo kwa kutembea umbali mrefu kutoka katika kata ya Ibanda.
Siku ya jumatatu kesho tarehe 08/01/2024, Kwa jitihada kubwa zilizofanywa na Mhe. Rais na Serikali yake ya awamu ya sita, Wanaibanda wanakwenda kuandika historia yakupata shule mpya ya Sekondari.
Asante Mama Tupo Tayari Kuwapokea wanafunzi wote tarehe 08/01/2024
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa