Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kata ya Ikama kijiji cha Ilopa kilichopo wilaya ya Kyela tarehe 15/7/204.
Katika ziara hiyo Mhe.Mkuu wa wilaya ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Bi. Florah Luhala, kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilopa Mhe. Mkuu wa wilaya, amewashukuru wananchi hao kwa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu kati ya kijiji cha Ilopa na Kyangala pia amesisitiza kudumisha amani katika vijiji hivyo.
Akijibu kero mbalimbali, ikiwemo suala umeme na maji Mhe. Mkuu wa wilaya amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutoa fedha kwaajili ya kuendeleza miradi hiyo.
Aidhaa katika suala la miundombinu, Mhe. Mkuu wa wilaya ameagiza wataalamu kutoka TARURA kutembelea maeneo yanayoathiriwa na mafuriko hasa kipindi cha mvua, ikiwemo kityeputyepu kilichopo kijiji cha Ilondo kufanyiwa tathimini ili kuanza utaratibu wa kuboresha eneo hilo.
Vilevile Mhe. Mkuu wa wilaya amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Ilopa, kwa kuomba kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kupitia bwawa la kafunde linalopatikana katika kijiji hicho na amewaahidi kuwaleta wataalam wa kilimo ili kujua usalama wake.
Pia amewataka wazazi wenye watoto wa kike walio wanafunzi kutimiza ndoto za watoto wao kwa kufuata sheria na taratibu zilizopangwa na serikali kuweza kukomesha vitendo vya rushwa pindi watoto wao wanapopewa ujauzito wakiwa bado shuleni .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Bi.Flora Luhala amewashukuru wananchi kwa kuajili walimu wanaojotolea katika shule ya msingi Ilopa, kutokana changamoto ya uhaba wa walimu uliopo katika shule hiyo.
Pia ameahidi kuongeza walimu shuleni hapo mara baada ya ajira za serikali zitakapotoka.
Vilevile amewaomba wazazi wa kijiji cha Ilopa kuanzisha mchango wa chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata huduma ya chakula wanapokua shuleni.
Kwa upande wake Judith Masasi kutoka taasisi ya kuzuia kupambana na rushwa (TAKUKURU), amewaomba wananchi wa kijiji cha Ilopa kufanya maaumuzi sahihi ya kuepukana na rushwa hasa kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa, ili waweze kupata viongozi bora watakaoweza kuwaongoza.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa