Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa amewasihi wananchi wa wilaya ya Kyela kuwahi kupata chanjo ya Corona mapema ili kuepuka foleni ndefu, Mhe. Mlawa ameyasema haya mapema leo tarehe 06/08/2021 wakati akizindua na kuchanja chanjo hiyo, katika hospitari ya wilaya ya Kyela.
Amesema wilaya ya Kyela imepewa chanjo 6000, Na kipaumbele kitatolewa kwa mwananchi yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 49 hii ni kwa wale wenye magonjwa sugu, pia itatolewa kwa mwananchi yeyote yule asiekuwa na magonjwa sugu na mwenye umri wa kuanzia miaka 50 nakuendelea pamoja na watumishi wa Afya.
Pia ameongeza kusema katika wilaya ya Kyela tutakuwa na vituo 3 vya utoaji wa chanjo hii, yaani Hospitali ya wilaya, kituo cha afya Ipinda na katika zahanati ya Njisi.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa