Boma la jengo la zahanati katika kijiji cha Masoko kata ya Busale, ikiwa zaidi ya shilingi milioni 18 zimechangwa na wananchi hadi kufikia ngazi linta.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amewapongeza wananchi wa kata ya Busale wilayani Kyela kwa umoja wao wa kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata yao.Mheshimiwa Mwenyekiti ameyazungumza haya alipowatembelea wananchi hao katika kijiji cha Busoka na kijiji cha Masoko siku ya tarehe 04/02/2022.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Masoko kata ya Busale hapa wilayani Kyela Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amesema, katika bajeti hii wamelingiza boma la zahanati ya kijiji cha masoko katika maombi maalumu ya kupatiwa fedha ili kulimalizia boma hilo ikiwa ni pamoja na maboma mengine 9 yaliyopo katika kata nyingine.
"Tunatambua wananchi wanataka matokeo hivyo kiongozi ni lazima uwe mkweli kwa wananchi ili yote tunayozungumza tuweze kuyatimiza kwa wananchi wetu ili wazidi kutuamini" alisema.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono aliweza kutembelea kijiji cha Busoka katika kata ya Busale na kuwaambia wanaBusoka anawapenda sana na anawapongeza sana kwa kuanzisha mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Busoka.
Pamoja na hayo Mheshimiwa Katule alisema, kwa mda mfupi tumeona Busale inakimbia sana kwa maendeleo, Aliwataka wanaBusoka kuendelea kushikamana na kufanya maendeleo. Pamoja na hayo Mheshimiwa alisema, Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suruhu Hassan haijawaacha wanaBusoka, na imeleta fedha kiasi cha shilingi 50,000,000/=.
Aidha aliwataka wanaBusoka kuendelea kujitoa katika kuchangia Zahanati yao ili kuikamilisha kwa wakati, na anaamini punde Zahanati itakapokamilika, Serikali italeta wataalam kwa kuanza kazi.
Akiongea kwa njia ya simu Mbunge wa Kyela Mheshimiwa Ally J. Kinanasi
Alisema atachangia anawapenda sana wananchi wa Busake na katika kuonyesha kuwa yupo pamoja na wananchi hao atachangia shilingi milioni 1 kwa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Masoko.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa