Wananchi wa kata ya Busale iliyopo katika wilaya ya Kyela, wamepata fulsa ya kuyembelewa na Waheshimiwa madiwani wa wilayani hapa, na kupewa pongezi nyingi kwa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa ikiwa ni kwa nguvu za wananchi pekee.
Ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari Kiwira coal mine, ambapo hadi kufikia hapo jumla ya shilingi 12,293,000/= zimetumika ikiwa ni nguvu za wananchi tu, ambao wanatimiza azma ya maendeleo yanayosisitizwa na serikali ya awamu ya tano.
Kwa kupitia kamati zao za kudumu Waheshimiwa madiwani walianza ziara zao za kutembelea miradi kuanzia tarehe 13/03/2020-17/03/2020, na Katina ziara hizo walipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa chumba cha mionzi (uletra) kinachojengwa katika kituo cha afya kilichopo katika kata ya Ipinda wilayani Kyela, pia waliweza kutembelea mradi wa ujenzi wa vyumba 4 katika shule ya msingi Mbala iliyopo katika kata ya Kajunjumele, ujenzi wa hosteli 2 na bwalo 1katika shule ya sekondari Kafundo iliyopo katika kata ya Ipinda, ujenzi wa zahanati katika kata ya Ipande pamoja na ujenzi wa stendi ya maegesho ya magari ikiwa ni sehemu ya chanjo cha mapato.
Aidha wakiwa katika ukarabati wa zahanati iliyopo katika kijiji cha Mpunguti kata ya Makwale iliyopewa shilingi 46,000,000/= na serikali kuu, kwa umaliziaji wa zahanati hiyo, Mhe. Hassan Mwambokela diwani wa kata ya Mkokwa wilayani hapa alisema pesa zote za umaliziaji wa jengo hilo ni lazima ziingizwe katika akaunti ya kijiji husika kama maagizo ya serikali kuu yanavyitaka. Hivyo waheshimiwa kwa pamoja walimtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Francis Mwaipopo kutimiza jambo hilo haraka.
umaliziaji wa ujenzi wa zahanati ya Mpunguti iliyopo katika kijiji cha Mpunguti kata ya Makwale ukiendelea, ambapo serikali kuu imetoa shilingi 46,000,000/= kwa umaliziaji huo.
Kamati zote za madiwani ziliweza kutoa pongezi za dhati kwa kampuni ya Bioland na Kim's chocolate ambazo zinanunua kakao hapa wilayani Kyela, kwa kazi kubwa zinazofanya kwa kukarabati na kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali wilayani hapa.
Ujenzi wa mabweni 2 na bwalo 1 katika shule ya sekondari Kafundo iliyopo katika kata ya Ipinda wilayani Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa