Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase ametembelea kata ya Talatala kijiji cha Ngolela tarehe 12/7/2024, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wilaya ya Kyela.
Katika ziara yake Mhe. Josephine Manase, ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Bi.Flora Luhala, Wakuu wa idara na Wakuu wa taasisi mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na wananchi wa kijiji cha Ngolelela Mhe. Josephine Manase, amewaomba wazazi kua na utaratibu wa kutoa mchango wa chakula kwa wanafunzi ili waweze kupata huduma ya chakula wanapokua shuleni.
Akisikiliza kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kero ya vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike, unaotokea kutokana na uwepo wa pori katika kijiji hicho;
Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela, amewataka viongozi kwa kushirikiana na wananchi kusafisha eneo la pori hilo ili kulinda usalama kwa watoto wa kike hasa wanapoenda na kutoka shule.
Aidha Mhe . Mkuu wa wilaya aliweza kujibu na kutatua baadhi ya kero zilizotajwa na wananchi ikiwemo kero ya umeme, miundombinu, na maji kupitia taasisi husika,
Aidha katika suala la ukosefu wa ajira amewataka wananchi waliohitimu kada mbalimbali kujiunga kwenye mfumo wa ajira na kufanya kazi kwa kujitolea kulingana na kada zao ili kupata ujuzi zaidi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Bi. Florah Luhala ametoa maagizo kwa walimu wanaondelea kuchangisha michango wanafunzi pasipo makubaliano rasmi baina yao na wazazi, kukomesha maramoja michango hiyo ikiwa ni kuendeleza sera ya elimu bure.
Pia kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa Bi. Flora Luhala amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura pindi itakapoanza zoezi hilo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa