Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Kata ya Bujonde Kijiji cha Isanga tarehe.11.7.2025.
Miongoni mwa kero zilizoongelewa ni kama kushuka kwa bei ya Kokoa,utoro wa Wanafunzi,ushuru kwa wakulima, na michango mashuleni.
Akizungumzia suala la michango mashuleni Mhe Mkuu wa Wilaya amesema Serikali inatoa Elimu bure hivyo ni jukumu la Wazazi kutoa mchango wa chakula na endapo kutakua na michango mingine tofauti ni lazima kuwe na makubaliano baina ya Walimu na Wazazi juu ya mchango huo.
Mkuu wa Wilaya amewataka Wazazi wenye watoto wanaosoma kuwa karibu na Watoto wao ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowasababishia Wanafunzi utoro na kukatisha masomo yao.
Mhe. Manase amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Isanga kwa jitihada za ujenzi wa zahanati ambayo ipo hatua ya Msingi, pia Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa Tsh 1,500,000 ambapo Tsh Laki tano (500,000) itatoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Tsh Million 1 (1,000,000) itatoka kwenye Mfuko wa Kokoa ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Wananchi katika ujenzi wa zahanati mpya ya Isanga.
Kuhusiana na changamoto ya kushuka kwa bei ya Kokoa,Mhe. Manase amevitaka vyama vya msingi (AMCOS) kutangaza bei mpya ya kokoa inayotolewa kwenye mnada wa mwisho unaofanyika kila wiki siku ya jumatatu ili wakulima waweze kujua bei halali itakayowasadia kuondokana na bei za mtaani.
Katika msimu huu wa mavuno Mhe.Manase amewahimiza Watendaji wa Kata kupatikana kirahisi kwenye maeneo yao ya kazi ili waweze kutoa vibali vitakavyowaondolea usumbufu wakulima pindi wanaposafirisha mazao yao.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa