Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera amehitimisha ziara yake Wilayani Kyela tarehe 10.6.2025 kwa kukagua mradi wa ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Kafundo,ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Makwale,Uzinduzi wa zahanati ya Kyangala pamoja na Uzinduzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Sekondari Ipinda.
Akizindua Zahanati ya Kyangala Mhe.Mkuu wa Mkoa ameupongeza Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita unaoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakufanikisha Ujenzi wa Zahanati ya kyangala na kutatua adha iliyodumu kwa muda mrefu kwa Wananchi wa Kijiji hicho katika kupata huduma za Afya kwa haraka
Aidha Zahanati ya Kyangala mpaka kukamilika kwake imegharimu kiasi cha Tsh. Millioni 142,125,000/= kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato:-
Michango kutoka kwa wananchi wa Kyangala 22,330,000/= ,Wadau wa Maendeleo 2,520,000/=, Mfuko wa Jimbo 7,300,000/= ,Fedha kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela 300,000/= ,Mchango wa kokoto kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Tsh.500,000/=, Fedha kutoka Serikali kuu Tsh. Milion 30,000,000, Fedha kutoka Halmashauri (Mapato ya ndani) Tsh.49,175,000/= Fedha kutoka Halmashauri (Mapato ya ndani) Milion 30,000,000/=
Hatahivyo Mradi huo wa Zahanati unatarajia kuhudumia Wananchi takribani 1071 wakazi wakijiji cha Kyangala na Wengine kutoka Vijiji jirani
Mhe.Homera amewaagiza wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARULA, kutafuta njia mbadala ya kurekebisha miundombinu ya barabara inayotoka Zahanati ya Kyangala kwenda kituo cha Afya Ipinda na kuwasilisha taarifa ya jitihada hiyo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ndani ya siku7 ,ili wananchi waweze kuyafikia matibabu kwa haraka.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza mkandarasi wa bweni la Shule ya Sekondari Kafundo kukamilisha ujenzi ifikapo tarehe 28 mwezi huu kwani Serikali itavunja mkataba na kuchukua hatua za kinidhamu endapo mradi huo hautakamilika.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa