Haya yamezungumzwa na Mkuu wa Idara ya Maji wa wilaya ya Kyela ndugu Amos Mtweve, alipokuwa akiongea katika kikao na Wananchi wa kitongoji cha Kilosi, kijiji cha Mpanda, kata ya Lupata wilayani Rungwe, tarehe 12/10/2018.
Kikao hicho kilifanyika kwa malengo yakuwataka wananchi hao kutunza mazingira ya chanzo cha mradi mkubwa wa maji utakaoanzia katika Halmashauri ya Busokelo, kata ya Kilosi hadi wilayani Kyela.
Aidha Wananchi walifurahishwa na taarifa ya utunzaji wa mazingira, katika chanzo hicho na kuahidi kujitolea mazingira yao yanayozunguka chanzo hicho, ili kuweza kupanda miti kuzunguka eneo hilo.
Mwisho Mwenyekiti wa kitongoji ndugu Ambungite l. Mwafungo, alimshukuru ndugu Amos Mtweve kwa kuitisha kikao hicho, pia alivitaja vituo vya ugawaji maji vitakavyowekwa katika kata hiyo, yaani kituo cha Mpunguti, Kanisani na Kapengele.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa