Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase, amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ya mwili ili kuilinda afya, ili kutopata maradhi.
Mhe. Manase Ameyazungumza hayo tarehe 25.05.2024, alipokuwa kwenye ziara ya uhamasishaji wa upandaji wa miti katika shule ya msingi Matema Wilayani Kyela. Ambapo Mhe. Mkuu wa wilaya amesema, wilay tunatarajia kupanda miti takribani 1,500,000 mpaka kufikia mwezi wa saba Mwaka huu.
Aidha Mhe. Manase amempongeza Bw. Plotemy Mwakanyamale kwa kudhamini shughuli nzima ya upandaji wa miti pamoja na mashindano ya mbio za ufukweni, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani katika harakati za Utunzaji Mazingira.
Vilevile Mhe. Josephine Manase amewataka walimu na viongozi kuweka utaratibu wa upandaji wa miti kwa wanafunzi ili kuweza kurithisha Utamaduni huu kwa vizazi vyetu, nakuifanya wilaya ya Kyela kuwa mfano wakuigwa katika utunzaji wa mazingira.
Pamoja na hayo Mhe. Manase ametoa umuhimu wa upandaji miti wilaya ya Kyela ikiwa ni pamoja na kuepuka athari zitokanazo na uharibifu wa mabadiliko ya tabia nchi.
Mwisho Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase amewasisitiza wananchi kutokata miti ovyo, kwani ni uharibifu wa mazingira, amewataka wananchi kujikita katika matumizi ya nishati safi na salama.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa