Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Kyela Ndg.Keneth Nzilano amefungua mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri tarehe 4.8.2025.
Mafunzo hayo yatafanyika ndani ya siku tatu mfululizo kwa washiriki 66 kutoka kata za Halmshauri ya Wilaya ya Kyela.
Ndg.Nzilano amewataka washiriki wa mafunzo kuzingatia katiba,Sheria kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Tume ya uchaguzi.
Aidha amewataka washiriki kutambua mapema vituo vya kupigia kura ili kubaini mahitaji maalumu ya vituo husika na kuhakikisha vinakua na mpangilio mzuri utakaoruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa