Akizungumza katika ufunguzi wa semina leo tarehe 6/06/2022, Semina ya uwasilishwaji wa matokeo utafiti na mafunzo ya ujasiriamali unaohusisha kilimo biashara, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mhe. Ismail Mlawa amesema,
Anashukuru sana wataalam utafitiwa kilimo biashata kutoka chuo kikuu cha Dara es salaam, kwa kufanya tafiti inayonesha ushiriki wa wanawake katika kilimo biashara, Na pia anaimani kwamba awamu ya pili ya tafiti hii itahusisha wanawake wengi zaidi ili elimu hii iweze kusambaa kwa kasi ndani na nje ya wilaya yetu ya Kyela.
Aidha amesema ni kweli wanawawake wengi ushiriki wao katika maswala ya kilimo biashara ni mchache sana, Lakini kwa kupitia elimu hii anaamini wanawake wengi watainuka na watashiriki katika shughuli za ujasiriamali na hatimae kuondoa unyonge wao katika unufaikaji wa mazao wanayyalima sawa na wanaume.
"Moja ya kazi ya Mkuu wa wilaya ni kuhamasisha maendeleo kwa wananchi, hivyo nitahakikisha elimu hii nami naipeleka kwa wananchi" Alisema Mhe. Mkuu wa wilaya. Mwisho alitoa shukrani kwa shirika la "SIDA" kwa udhamini wa kuafanya utafiti huu katika wilaya ya Kyela.
Nae Prof. Lehice Kinundwa Rutashobya kutoka Chuo Kikuu Dar es salaam amesema, anamshukuru sana Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela kwa kujitoa na kufika katika uwasilishwaji huu wa mradi wa kilimo biashara kwa maendeleo, Pia Amesema mradi huu ni muhimu sana katika nchi yetu kwa sababu mradi huu unakwenda kumsaidia wanawake wote.
Hata hivyo katika nchi ambazo zinaendelea katika kilimo biashara wanawake wengi wapo nyuma sana katika kupata faida ya mazao ya kilimo, hasa ukizingatia wanawake wengi ndio wanaotunza familia.
Amesema mradi umebaini kuwa wanawake hawashiriki sana katika kufaidika na matunda ya kilimo. Sasa mradi huu una lengo kubwa la kufanya tafiti ya shughuli za kilimo bishara katika wilaya ya Kyela ili kutoa elimu kwa wanawake na mwishoe waweze kufaifika na kilimo.
Akitoa neno la shukrani Dr. Tumsifu Elly amesema, anatoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ya Kyela kwa kuelewa haraka malengo ya mradi huu, ambao unalenga kuinua mnyororo wa thamani katika soko la mazao, katika wilaya ya Kyela na Taifa kwa ujumla.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa