Watumishi wa Afya watoa mafunzo juu ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi tarehe 17/04/2024, mafunzo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Kyeladay hapa wilayani Kyela.
Aidha mafunzo hayo yamefanyika kwa walimu wa afya kutoka sekondari 35 na shule ya msingi 107.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu wa afya 151 pamoja na wachanjaji 43 ili waweze kwenda kufanya kampeni ya kuchanja HPV.
Walengwa ni wasichana miaka 9 hadi 14. Hapo awali chanjo hii ilikuwa inatolewa kwa wasichana miaka 14 tuu.Wizara ya afya imeongeza Umri, kwa sasa itatolewa kwa wasichana miaka 9 hadi 14 ili kuwakinga wasichana hawa na saratani ya mlango wa kizazi.
Pia chanjo hii kwa sasa itatolewa dozi 1 tuu na Msichana atakuwa tayari na kinga kamili ya saratani ya mlango wa kizazi.
Walimu wanatakiwa kusajili wasichana hao kwenye rejesta maalumu kuanzi tarehe 18 na 19 ya mwezi wa 4 2024.
Uchanjaji utaanza Rasmi tarehe 22.04.2024 hadi 26.04.2024 hivyo ni vyema Walengwa wote wakafikiwa.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa