Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Idara ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na lishe(W) Dkt. Saumu Kumbisaga alipokuwa akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani iliyofanyika tarehe 12/05/2023 katika viwanja vya hospitali ya wilaya ya Kyela.
Daktari Kumbisaga amewataka wauguzi kuwa na lugha rafiki kwa wagonjwa hasa kwa akina mama wajawazito, ili kuwaongezea amani na kuwafanya wajifungue kwa salama.
Aidha amewataka wauguzi kujiamini na kufanya kazi kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu, kwani bila wao hakuna daktari.
Kwa wale watumishi wachache ambao wameingia katika fani ya uuguzi, Ili kutafuta ajira na si kusaidia wagonjwa, amesema hao ndio wanaoharibu sifa ya kazi za wauguzi na ameahidi kuwaibua watumishi hao wasiokuwa na lugha rafiki kwa wagonjwa, bila kusubiri viongozi kuwaibua watumishi hao.
Pamoja na hayo Dkt. Kumbisaga amewataka watumishi wote wanaojitolea katika Idara ya afya, wafanye kazi kwa miongozo ya afya na kwa nidhamu kubwa, kwani hata zinapotokea ajira wao wanakuwa mstari wa mbele katika kuwasemea.
Pia Dkt. Kumbisaga ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuajiri watumishi wengi katika kada hii ya afya.
Pongezi nyingine amezipeleka kwa wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Kyela, kwani kwa sasa imeanza kusifiwa kwamba huduma zimeboreshwa.
"Sisi waauguzi tumesomea kutibu, hatujasomea kuua, tunatoa huduma ya kutibu wagonjwa hivyo wananchi wawe na amani wanapofika hospitari" amesema Dkt. Kumbisaga.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa